Uongozi wa klabu ya Yanga umemwongezea majukumu kocha wao
mpya, Hans Van Der Plyum raia wa Uholanzi kwa kumpa cheo cha Mkurugenzi
wa Ufundi huku ukimtaka awasilishe kwa maandishi ripoti yake kila wiki.
Plyum ambaye amesaini mkataba wa miezi sita kuinoa Yanga
ambao utamalizika Juni 30, tayari amejiunga na kikosi hicho
kilichopo kambini nchini Uturuki, ambapo kilikuwa chini ya kocha
msaidizi, Charles Boniface Mkwasa.
Akizungumza jijini jana, Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga,
Clement Sanga alisema wameamua kumpa Ukurugenzi wa Ufundi kocha huyo
wakiamini kuwa anaweza kufanya kazi yake kama
kocha na kutekeleza majukumu hayo mengine ndani ya klabu.
“Tunamwamini kocha wetu mpya, anaweza kutekeleza
majukumu yake, lakini tunachokitaka ni uongozi kuwa karibu na benchi la
ufundi na tulichokiamua ni kocha kutuletea ripoti ya mwenendo wa timu
tena kwa maandishi na siyo kwa maneno kama ilivyokuwa awali kila wiki,”
alisema Sanga

haya young afreican
ReplyDelete