Tuesday, 18 February 2014

YANGA YAMPA CHEO KINGINE KOCHA WAO

Uongozi wa klabu ya Yanga umemwongezea  majukumu kocha wao mpya, Hans Van Der Plyum raia wa Uholanzi  kwa kumpa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi huku ukimtaka  awasilishe kwa maandishi ripoti yake kila wiki.
Plyum ambaye amesaini mkataba wa miezi sita kuinoa Yanga ambao  utamalizika Juni 30, tayari amejiunga na kikosi hicho kilichopo  kambini nchini Uturuki, ambapo kilikuwa chini ya kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa.
Akizungumza jijini jana, Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga alisema wameamua kumpa Ukurugenzi wa Ufundi  kocha huyo wakiamini kuwa anaweza kufanya kazi yake kama kocha  na kutekeleza majukumu hayo mengine ndani ya klabu.
“Tunamwamini kocha wetu mpya, anaweza kutekeleza majukumu  yake, lakini tunachokitaka ni uongozi kuwa karibu na benchi la ufundi  na tulichokiamua ni kocha kutuletea ripoti ya mwenendo wa timu tena  kwa maandishi na siyo kwa maneno kama ilivyokuwa awali kila wiki,” alisema Sanga

1 comment:

AJALI YA MOTO SHULE YA OLD TANGA

Ajali ya moto yatokea shule ya sekondari old tanga leo tarehe 18/09/2019 mchana.kwa mujibu wa kamanda wa polisi chanzo cha ajali hiyo a...